Ujumbe kutoka kwa Mkuu wa Chuo
Chuo Kikuu cha Kikristo Elam (ECU)
ni Taasisi ya Elimu ya Juu ya Mafunzo ya Kidini (Theolojia) Chuo hiki kwa kifupi kinajulikana kwa jina la
ECU ambalo ni kifupi cha Elam Christian
University. Chuo hiki kinatoa mafunzo
katika fani mbalimbali za kidini kwaajili ya kwatayarisha viongozi watumishi
kwaajili ya mavuno ya nyakati za mwisho.
Chuo hiki kina usajili wa kimataifa
kutoka katika bodi ya Kimataifa YA Usajili
wa Vyuo vya Biblia na Theolojia inayojulikana kwa jina la the Association Independent Christian
Colleges and Seminaries (AICCS) iliyoko Marekani. Kimesajiliwa kwa namba za
usajili 219120M. Vyeti
vinavyotolewa na Chuo hiki vinatambuliwa kimataifa.Elam Christian University ni
Taasisi isiyo ya kibiashara inayotoa mafunzo yenye ubora wa kitaifa na
kimataifa katika kuwatayarisha viongozi watumishi.
ECU
inatoa mafunzo yasiyoegemea kwenye dhehebu lolote lile, bali mafunzo
yenye msingi wa Ki-Biblia yenye kuwatayarisha
viongozi watumishi katika nyanja zote yaani kiroho, kimwili na kiakili ili kuwezesha kila kiongozi mtumishi kutimiza
kwa ufanisi kusudi la wito wake. Mafunzo
yanayotolewa katika chuo hiki ni nusu nadharia na nusu vitendo, mwanafunzi anahimizwa kuyaweka
katika vitendo yale ajifunzayo darasani.
Elam Christian University ni Chuo
chenye wakufunzi na Wahadhiri mahiri ambao wamebobea katika kazi ya ufundishaji
katika elimu ya Theolojia na huduma.
Chuo hiki ni cha Kipentekoste na kinafanya kazi na madhehebu yote ya
Kikristo yenye kukubaliana na maono yake. Chuo hiki pia kinapokea wanafunzi wa
rangi, dini, jinsi zote kutoka katika
madhehebu na taasisi mbalimbali za kidini.
Pia chuo hiki kinapokea wanafunzi kutoka katika mataifa mbalimbali
duniani na kuwatarisha katika maeneo ya huduma ili waweze kuleta athali katika ulimwengu na kutimiza
kusudi la wito wa kila mmoja wao.
Kwa niaba ya jumuiya ya Chuo Kikuu
cha Kikristo Elam ninakukaribisha kwa moyo mkunjufu katika chuo hiki
na ninafurahi kwamba unafikiria kujiunga nasi kwa masomo yako katika
chuo hiki. Chuo Kikuu cha Christian Elam ni Chuo Kikuu cha Biblia, Theolojia na Uongozi, kinachojulikana sana kwa viwango
vya juu zaidi vya ufundishaji na ujifunzaji. Maono yetu ni kutambuliwa kama
taasisi ya Kidini inayoongoza ulimwenguni kwaajili ya
utayarishaji wa viongozi watumishi na Watendakazi waliokidhi vigezo vya kitaifa
na kimataifa katika kutumikia kusudi la
Mungu duniani.
Chuo hiki kina kampasi na vituo vya
mafunzo ndani na nje ya nchi. Chuo kina vituo vya mafunzo katika mikoa
mbalimbali hapa Tanzania. Pia chuo hiki kina kampasi katika nchi za Malawi,
Zambia, Kongo DR, Kenya. Pia chuo kinaendelea kufungua kampasi katika nchi
mbalimbali duniani.
Chuo hiki kinatoa mafunzo kuanzia
ngazi ya Atashahada (cheti) hadi ngazi ya Shahada ya Uzamivu (PhD) katika fani
zifuatazo: Theolojia na Biblia, Theolojia na Huduma za Kanisa, Elimu ya
Kikristo, Theolojia na Ushauri wa Kichungaji, Theolojia na Uongozi wa Kanisa, Kupanda
Makanisa na Umisheni wa Ulimwengu, Uteteaji wa Imani ya Kikristo na uamsho na mabadiriko ya Kiroho
Chuo hiki kimetayarisha mitaala ya
mafunzoywenye kukidhi ubora wa kitaifa na kimataifa unaoweka mkazo zaidi katika utendaji kuliko
nadharia na unao mwandaa mwanafunzi katika maeneo au Nyanja zote ili kuleta
ufanisi katika huduma.
Chuo hiki kinatoa mafunzo kwa njia ya ana kwa ana (darasani)
na kwa njia ya masafa. Kwa wanafunzi wanaosoma kwa njia ya ana kwa ana wanafunzi huhudhuia
mafunzo katika vituo vilivyoko katika mikoa na nchi mbalimbali. Kwa wanafunzi
wanaosoma kwa njia ya masafa mafunzo hutolewa kwa njia ya mtandao na kwa njia
ya posta. Wanafunzi wanaosoma kwa njia ya mtandao huhudhiria mafunzo kupitia
madarasa ya mtandaoni yaani mikutano ya
zoom, watsapp na Telegram. Kila mwanafunzi huchagua mfumo wa kusoma kulingana
na mazingira yake.
Mwongozo wa mafunzo ambao uko katika
tovuti hii utakuongoza kuchunguza
masuala muhimu ya kitaaluma na kiutawala. Muhimu zaidi utakuongoza kupitia
programu, muundo wa kozi na yaliyomo, wafanyakazi, na maelezo ya vifaa vya
ustawi wa wanafunzi na pia kukuongoza kupitia michakato ya maombi na
uandikishaji. Tunakuhimiza ujiunge nasi kwa masomo yako zaidi. Ikiwa kwa bahati
yoyote kuna changamoto katika kutumia
Mwongozo wa Mafunzo (prospectus) tafadhali wasiliana nasi kwa ufafanuzi
zaidi.
Napenda kutumia nafasi hii
kukujulisha kwamba hujatembelea kwa bahati mbaya tovuti hii bali kwa kusudi
takatifu la Mungu ili uweze kupata ufahamu kuhusu Elam Christian University na
kisha ufanye aauzi ya kujiunga na chuo hiki
Napenda kukukaribisha kujiunga na mafunzo katika chuo chetu
ili uweze kuandaliwa kaa kiongozi mtumishi katika kutumikia kusudi la Bwana
wetu Yesu Kristo. Hakika hutabaki ulivyo baada ya kuhudhuria mafunzo haya. Napenda kukuhakikishia kuwa
hutajuta kusoma katika chuo hiki.
Ni mimi ndugu yako,
Rev.Prof.
Erick L.Mponzi (ThD)
MKUU WA CHUO