DIGRII YA KWANZA YA THEOLOJIA KWA KISWAHILI
SHAHADA YA KWANZA YA THEOLOJIA KWA KISWAHILI
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Elam Christian University (ECU) anapenda kuwatangazia wakristo wote na wachungaji nafasi za kujiunga na masomo ya Shahadaya Kwanza (Bachelor Degree ) ya Biblia na Theolojia (BBT) kwa lugha ya Kiswahili. Digrii ya Kwanza ya Biblia na Theolojia ni program maalumu ambayo imeandaliwa kwaajili ya wanafunzi ambao hawana ujuzi wa lugha ya kiingereza. Lugha haipaswi kuwa kikwazo cha kuzuia watu kutotimiza ndoto zao za kielimu. Wataalamu wa isimu wanathibitisha kwamba mtu anapojifunza kwa lugha yake anaelewa zaidi kuliko mtu anaejifunza kupitia lugha ya kigeni.
Kwa kutambua hayo Baraza la chuo limepitisha azimio la kuanzishwa kwa kwa program ya Shahada ya kwanza ambayo itafundishwa kwa lugha ya Kiswahili
Programu hii inalenga kumjengea mwanafunzi uwezo, stadi na ujuzi katika Biblia, Theolojia, Huduma na uongozi wa kiroho ili kumwezesha mwanafunzi kuwa na ufanisi katika huduma na kuweza kukabiliana na kuzishinda changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika huduma na katika maisha ya kiroho kwa ujumla.
Program hii itamuwezesha mwanafunzi kuwa na uelewa wa juu zaidi wa Biblia na Huduma na mwanafunzi ataweza kuhubiri na kulifasiri Neno la Mungu kwa usahihi zaidi.
Programu hii ya Shahada ya Kwanza ya Biblia na Theolojia kwa Kiswahili inatolewa katika vituo vyetu vya mafunzo vilivyoko katika mikoa mbalimbali hapa nchini na nchi za nje.
Pia masomo haya ya shahada ya Kwanza kwa lugha ya Kiswahili yanatolewa kupitia Elimu masafa yaani mwanafunzi ambae hana muda wa kukaa darasani ataweza kusoma kwa njia ya mtandao au posta na kufikia malengo yake ya kupata Digrii ya Kwanza ya Theolojia
Elam Christian University ni Chuo ambacho kina usajili wa kimataifa na kina wakufunzi na wahadhiri mahiri waliobobea katika ufundishaji na huduma. Vyeti vyote vinavyotolewa na chuo hiki vinatambuliwa kitaifa na kimataifa.
Chuo kimetoa ofa kwa wanafunzi wote watakaojunga na program hii chuo kitawafadhili 50% ya Ada ya mafunzo . Wanafunzi watalipa ada 50% mpaka wanahitimu mafunzo yao.
Muundo wa programu
Idadi ya kozi mwanafunzi anazotakiwa kusoma inatofautiana kulingana na sifa za kuingilia kama ifuatavyo:-
Mwanafunzi mwenye Diploma ya Theolojia atasoma kozi 35
Mwanafunzi mwenye Shahada ya Sekyura atasoma kozi 25 na kuandika tasnifu moja
Mwanafunzi mwenye Diploma ya Sekyura atasoma kozi 42
Sifa za kujiunga
Mwombaji anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:-
1. Awe mwamini wa kanisa la mahali pamoja (local congregation) asiwe mwongofu mpya
2. Awe na umri wa kuanzia miaka 21 na kuendelea
3. Awe na Stashahada au Shahada yoyote kutoka katika chuo kinachotambuliwa na chuo hiki
4. Awe na wito wa kumtumikia Mungu
5. Awe tayari kufuata sheria kanuni na taratibu zote za Elam Christian University
6. Awe na uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiswahili Fasaha.
Namna ya kujiunga
Fomu za Kujiunga zinapatikana katika vituo vyetu vya mafunzo vilivyoko katika mikoa mbalimbali
Pia unaweza kupata fomu kupitia mtandao tembelea tovuti yetu www.elamcuedu.org
Mwanafunzi atapaswa kulipia ada ya kujiunga kabla ya kujaza fomu
Muda wa kujiunga na mafunzo haya ni muda wote
piga simu 0762532121 au 0753636722 kwa maelezo zaidi
Gharama za mafunzo
Na |
Aina Ya Malipo |
Kiasi (Tsh) |
01. |
Fomu ya Kujiunga |
35,000/= |
02. |
Udhibiti ubora wa Elimu (inalipwa mara moja tu kwa mwaka) |
35,000/= |
03. |
Uendeshaji wa Shule ya Shahada za Awalli Elimu (inalipwa mara moja tu kwa mwaka) |
35,000/= |
04. |
Kitambulisho cha Mwanafunzi |
15,000/= |
05. |
Ada kwa kila kozi (somo) 115,000/= baada ya punguzo la ufadhili mwanafunzi analipa |
65,000/= |
06. |
Mazoezi ya vitendo (awamu mbili ) kila awamu |
65,000/= |
07. |
Usimamizi wa tafiti |
115,000/= |
08. |
Ada ya cheti baada ya kufuzu mafunzo |
125,000/= |
ORODHA YA KOZI ZA SHAHADA YA KWANZA BIBLIA NA THEOLOJIA
MWAKA WA KWANZA Semista ya Kwanza |
|||||||
NAMBA YA KOZI |
JINA LA KOZI |
KREDITI |
HADHI |
||||
EBA 0111 |
Stadi za Mawasiliano na Mbinu za Kujifunza |
2 |
Lazima |
||||
EBT 0112 |
Utangulizi wa Biblia |
3 |
Lazima |
||||
EBB 0113 |
Pitio la Agano la Kale |
3 |
Lazima |
||||
EBB 0114 |
Pitio la Agano Jipya |
3 |
Lazima |
||||
EBT 0115 |
Misingi ya Imani |
3 |
Lazima |
||||
EBM 0116 |
Kuisikia sauti ya Mungu |
3 |
Lazima |
||||
EBB 0117 |
Kujifunza Biblia kwa Ubunifu I |
3 |
Lazima |
||||
EBT 118 |
Utangulizi wa Theolojia |
2 |
Lazima |
||||
EBT 0119 |
Sikukuu za Bwana |
3 |
Lazima |
||||
EBM 01110 |
Ndoa na Familia |
3 |
Lazima |
||||
EBL 01111 |
Uongozi na Utawala |
3 |
Lazima |
||||
Semista ya pili |
|||||||
NAMBA YA KOZI |
JINA LA KOZI |
KREDITI |
HADHI |
||||
EBB 0121 |
Kujifunza Biblia kwa Ubunifu II |
3 |
Lazima |
||||
EBT 0122 |
Kukuza Mtazamo wa Ulimwengu wa Biblia |
3 |
Kuchagua |
||||
EBT 0123 |
Pneumatolojia |
3 |
Lazima |
||||
EBM 0124 |
Mikakati ya Mavuno ya Kiroho |
3 |
Kuchagua |
||||
EBT 0125 |
Theolojia ya Maagano |
3 |
Lazima |
||||
EBT 0126 |
Theolojia ya Nyakati |
3 |
Lazima |
||||
EBL 0127 |
Kanuni za Kufaulu na Kufanikiwa Ki-Biblia |
3 |
Kuchagua |
||||
EBT 0128 |
Theolojia ya Kimfumo III |
3 |
Lazima |
||||
EBM 0129 |
Mazoezi ya Vitedo I |
2 |
Lazima |
||||
Semista ya tatu |
|||||||
NAMBA YA KOZI |
JINA LA KOZI |
KREDITI |
HADHI |
||||
EBB 0231 |
Injili Zinazolandana |
3 |
Kuchagua |
||||
EBA 0232 |
Utangulizi wa Saikolojia |
3 |
Lazima |
||||
EBL 0233 |
Utawala wa Kanisa |
3 |
Lazima |
||||
EBT 0234 |
Theolojia ya uwakili |
3 |
Kuchagua |
||||
EBL 0235 |
Kiongozi wa Kanisa mwenye ufanisi |
3 |
Lazima |
||||
EBT 0236 |
Theolojia IV |
3 |
Lazima |
||||
EBM 0237 |
Historia ya kanisa la Afrika |
3 |
Kuchagua |
||||
EBM 0238 |
Historia ya kanisa III |
3 |
Kuchagua |
||||
EBM 0239 |
Agizo Kuu |
3 |
Kuchagua |
||||
EBM 02310 |
Uongozi na umisheni I |
3 |
Kuchagua |
||||
EBM 02311 |
Uongozi na Umisheni II |
3 |
Kuchagua |
||||
EBM 02312 |
Vita vya Kiroho I |
3 |
Kuchagua |
||||
EBM 02313 |
Mazoezi ya Vitendo II |
2 |
Lazima |
||||
EBT 02314 |
Dini za Ulimwengu |
3 |
Kuchagua |
||||
MWAKA WA PILI Semista ya Nne |
|||||||
NAMBA YA KOZI |
JINA LA KOZI |
KREDITI |
HADHI |
||||
EBM 0241 |
Huduma yenye nguvu |
3 |
Kuchagua |
||||
EBM 0242 |
Upako wa Roho Mtakatifu |
3 |
Kuchagua |
||||
EBT 0243 |
Kanuni za Kfasiri Maandiko |
3 |
Lazima |
||||
EBM 0244 |
Kanuni za Kuandaa Mahubiri |
3 |
Lazima |
||||
EBM 0245 |
Utangulizi wa Umisheni |
3 |
Kuchagua |
||||
EBT 0246 |
Ekklesiolojia |
3 |
Kuchagua |
||||
EBM 0247 |
Kupanda makanisa |
3 |
Kuchagua |
||||
EBM 0248 |
Vita vya Kiroho II |
3 |
Kuchagua |
||||
EBT 0249 |
Mbinu za utafiti wa Ki-Theolojia |
3 |
Kuchagua |
||||
EBM 02410 |
Huduma ya Kichungaji |
3 |
Kuchagua |
||||
EBT 02411 |
Eskatolojia |
3 |
Lazima |
||||
EBT 02412 |
Utafiti wa Ki-Theolojia |
3 |
Lazima |
||||
EBM 02413 |
Ushauri wa Kichungaji |
3 |
Lazima |
||||
Imetolewa na
Naibu Makamu Mkuu wa chuo Taaluma (DVCA)
ELAM CHRISTIAN UNIVERSITY