DIGRII YA PILI (UZAMILI) YA THEOLOJIA KATIKA UONGOZI
I.
DIGRII YA PILI YA THEOLOJIA KATIKA UONGOZI
(The Degree of Master of Theology in Leadership)
MAELEZO YA MTAALA
Shahada ya Uzamili katika Theolojia ni program ya Mafunzo ya Juu ya Theolojia katika uongozi ambayo yameandaliwa kwa minajili ya kuwatayarisha watumishi wabobezi wa Huduma na Uongozi. Programu hii imeandaliwa kwa lengo la kuziba pengo la ukosefu wa Viongozi wa Makanisa au huduma waliofunzwa na kubobea katika maswala ya Kitheolojia, huduma na uongozi.
Ni ukweli usiopingika kwamba miradi mingi inayoanzishwa na makanisa mengi ya kiroho huwa haifiki mbali na makanisa mengine yameshindwa kuwa na miradi ya maendeleo ndani ya kanisa au huduma na kubaki kutegemea mifuko ya waumini kama chanzo pekee cha mapato ya kanisa. Katika program hii viongozi wa kanisa watajifunza mambo muhimu sana kama vile namna ya kutumia Theolojia kama nyenzo ya kuikomboa jamii, kiroho, kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na Kijamii.
Pia viongozi wa kanisa watajifuunza kwamba taasisi wanazoziongoza ni kubwa kuliko wao. Maamuzi wanayoyafanya leo yanaathili kesho ya taasisi hizo. Hivyo watajifunza namna ya kupanga kwa kuweka malengo ya muda mfupi na muda mrefu. Namna ya kusimamia na kuratibu mipango, namna ya kusimmaia miradi mbalimbali ya taasisi na usimamizi wa fedha. Pia viongozi watajifunza namna ya kusimamia raslimali watu yaani wafanya kazi ndani ya taasisi. Taasisis ni matokeo ya uwepo wa watu hivyo ni lazima kuwa na usimamizi bora wa raslimali watu ili kuwepo na ustawi na uimara wa taasisi.
Pia matumizi ya Teknolojia katika kukuza na kueneza kanisa au huduma kiroho, kitakwimu na kijiografia. Pia kuwajengea watumishi na viongozi wa makanisa kuiona huduma kama kazi nyeti na si kuichukulia kama kazi ya ziada.
II. MALENGO YA JUMLA YA MAFUNZO
Kuwatayarisha viongozi watumishi wenye ujuzi na ubobezi katika huduma na uongozi kwaajili ya ustawi wa watu wa Mungu (kanisa) na taasisi wanazoziongoza au kuzisimamia. Kuinua jeshi la viongozi watakaofanya kazi ya Mungu kwa Roho na kwa akili pia. Kujenga kizazi kipya cha viongozi ambao watasaidia kukua na kuimarika kwa waamini na kusababisha taasisi zao kukua bila kuwalemea waumini. Kuwafanya viongozi wa Makanisa kuwa wabunifu na kuwa chanzo cha amani katika taasisi zao na taifa kwa ujumla.
III. MATOKEO YA KUJIFUNZA
Baada ya kujifunza program hii mwanafunzi ataweza
· Kusimamia maendeleo ya kanisa na jamii kwa ujumla katika Nyanja zote. Kisiasa, kiuchumi,kiutamaduni na kijamii.
· Kufundisha katika vyuo vya Biblia na Theolojia
· Kufanya kazi za utawala na uongozi katika taasisi. Mfano kuwa mkurugenzi au afisa tawala/mipango
· Kusimamia miradi mbalimbali ya taasisi
· Kuwa mshauri wa tasisi mbalimbali
IV. IDADI YA KOZI NA UTARATIBU WA KUJIFUNZA
Program ya Theolojia katika uongozi ina jumla ya kozi 16 na Tasnifu Moja yenye jumla ya krediti 54. Ambayo ni mafunzo ya miaka miwili ambayo yatafundishwa kwa mwaka mmoja. Kozi za mwaka wa kwanza ambazo katika usomaji zinasomwa kama muhula wa kwanza mwanafunzi atasoma kozi 8 mwanafunzi atachukua kozi zote za lazima na kuchagua kozi nyingine kadhaa kutoka katika kundi la kozi za kuchagua ili kukamilisha idadi ya kozi 8.
Pia katika kozi za mwaka wa pili ambazo katika usomaji ni kozi za muhula wa pili. Mwanafunzi atasoma kozi zote za lazima na kuchagua baadhi ya kozi kutoka kwenye kundi la kuchagua ili kukamilisha kozi 8.
Baada ya kumaliza kujifunza muhula wa kwanza mwanafunzi atatakiwa kuanza kuandika tasnifu. Kama mahitaji ya lazima ya kutunukiwa shahada ya Uzamili ya Theolojia katika uongozi (Master of Theology in Church Leadership). Wakati mwanafunzi anamaliza kujifunza kozi za muhula wa pili pia atakuwa anakamilisha kazi ya utafiti nah ii itamwezesha kukamilisha program ya masomo ya Shahada ya uzamili kwa mwaka mmojatu badala ya miaka miwili.