Mahafali ya ECU Mbeya Mjini

Mahafali ya ECU Mbeya Mjini
Bwana Yesu apewe sifa
Mkuu wa Chuo anapenda kuwatangazia wahitimu wa ngazi mbalimbali katika chuo hiki cha ECU na wanajumuiya wote wa ECU mahafali ya Saba sehemu ya nne ambayo itafanyika mnamo tarehe 22/12/2021 katika ukumbi wa Ibada wa kanisa la PENTECOSTAL HOLINESS MISSION yaani PHM forest Mbeya Mjini mkabala na chuo cha ufundi Moraviani.
Wahitimu wote wa vituo vya Mbeya na kutoka vituo vingine ambao mmefuzu masomo yenu mnakaribishwa kuja kushiriki mahafali haya. Mahafali haya yatakuwa ni mahafali ya mwisho katika mwaka huu wa 2021. Utaratibu wa namna ya kushiriki mahafali utatolewa muda si mrefu.
Mungu awabariki sana
Imetolewa Kurugenzi ya Mawasiliano na mahusiano ya Umma
ECU -HQ
Share :

Add New Comment

 Your Comment has been sent successfully. Thank you!   Refresh
Error: Please try again