TAARIFA KWA UMMA WOTE WA ELAM CHRISTIAN UNIVERSITY

TAARIFA KWA UMMA WOTE WA ELAM CHRISTIAN UNIVERSITY
Makamu Mkuu wa Chuo anapenda kuwajulisha umma wote wa Elam Christian University kwamba Mkuu wetu wa Chuo ametunukiwa rasmi renki ya uprofesa katika mahafali ya saba ya sehemu ya pili ya chuo chetu iliyofanyika Katika Kito cha Kinondoni mnamo tarehe 20/11/2021.
Hivyo basi Mkuu wetu wa chuo anatambuliwa rasmi kwa jina la Reverend Professor Erick L Mponzi kwa kifupi atatajwa kwa jina la Rev.Prof. Erick L Mponzi kuanzia sasa.
Pia mkuu Makamu Mkuu wa Chuo anapenda kuwajulisha kwamba Mhadhiri wetu na Mkurugenzi wetu wa utafiti na ushauri Rev. Angumbwike A Mwamtobe amefuzu na kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Theolojia katika Eklesiolojia katika mahafali yetu ya saba sehemu ya pili iliyofanyika Kinondoni jijini Dar ea Saalam mnamo tarehe 20/11/2021
Hivyo basi Rev. Angumbwike A Mwamtobe atatambuliwa kwa jina la Rev.Dr. Angumbwike A. Mwamtobe kuanzia tarehe 20/11/2021.
Wanafunzi na watumishi wote wa chuo kwa ujumla tunapaswa kuzingatia itifaki ya utambulisho pindi tunapowataja watumishi hao tuzingatie hadhi zao. Biblia inasema anaestahili heshima apewe heshima yake na anaestahili hofu apewe vivyo hivyo.
Ni matumaini yangu kuwa tutazingatia itifaki ya utajaji majina wakati wa mawasiliano ya aina zote kwa maandishi na kwa mdomo.
Nawatakia majukumu mema katika kuujenga mwili wa Kristo.
Imetolewa na
MKURUGENZI WA MAWASILIANO NA MAHUSIANO YA UMMA
ELAM CHRISTIAN UNIVERSITY
Share :

Add New Comment

 Your Comment has been sent successfully. Thank you!   Refresh
Error: Please try again